音效
		
		
		界面
		
		
		
	难度等级
	
	
	
		口音
		
				
				界面语言
				 
			 
			
			
			
			
		 
	 
	
	1
	
	
	
		
			
			 
			
			
			
			和/或在社交方面支持我。网络:
			
			
		 
	
	
		
	
	
	
    Nitarejea
    
    
    Vipi mizigo umeshaweka tayari  Sijechelewa nkaachwa na gari  Basi jikaze usilie mpenzi  Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi   Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna  Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna  Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina  Nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka tumaa   Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea  Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea   Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi  Ukumbuke na moyo utajawa na simanzi  Ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke yangu honey  Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah  Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani  Sina wakunitua nyumbani ntaliaa   Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo  Hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo  Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh  We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh   Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea  Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea   Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi  Usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki  Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki  Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki   Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi  Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ooh  Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki  Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki   Ntarejea mama  Niombee nirude salama  Ohhh watoto wadanganye  Ihh, ohh   Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea  Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea  Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea  
 
完毕